#Local News #Sports

KIKOSI CHA CHATAJWA

Kocha mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy ametangaza kikosi chake cha muda kwa ajili ya Michuano ya CAF ya Mataifa ya Afrika (CHAN) ambayo ni ya kipekee kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani.

Wanaoongoza kwa mashambulizi ni wafungaji bora wa ligi kuu iliyokamilika majuzi, Moses Shuma, Emmanuel Osoro na Ryan Ogam, ambao wametikisa nyavu mara 17, 16 na 15 mtawalia msimu huu. Mshambulizi wa Sofapaka Edward Omondi pia ameitwa kufuatia kampeni kubwa kwa klabu yake.

Katika safu ya kiungo, Mohammed Bajaber wa Kenya Police FC anaongeza cheche za ubunifu, huku mara ya kwanza timu ya taifa ikiwaita Keith Imbali na wachezaji wawili wa Ulinzi Stars Yakeen Muteheli na Staphod Odhiambo ni miongoni mwa nyuso mpya zilizojumuishwa kikosini.

Huu utakuwa ushiriki wa kwanza wa Kenya katika mashindano ya CHAN na timu hiyo inatazamiwa kuingia kambini mnamo Julai 10, 2025.

Kenya itaanza kampeni yake ya CHAN 2024 dhidi ya DR Congo mnamo Agosti 3 katika uwanja wa Kasarani, kabla ya kumenyana na Angola, Morocco, na Zambia katika hatua ya makundi.

Kwa mara ya kwanza katika historia, CHAN itaandaliwa pamoja na Kenya, Uganda, na Tanzania.

Michuano hiyo itaanza Agosti 2 hadi Agosti 30, 2025, na inaahidi kuwa sherehe ya kusisimua ya vipaji vya soka vya ndani kote Afrika Mashariki.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KIKOSI CHA CHATAJWA

GOR YAACHILIA WACHEZAJI WAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *