WAKAZI WEBUYE ‘HAWATAKI’ TRELA
Wakaazi wa eneobunge la webuye magharibi wanataka serikali kupiga marufuku trela za kusafirisha mizigo dhidi ya kutumia barabara ya Bokoli hadi matisi, wakisema malori hayo yamechangia kuharibika kwa barabara hiyo mbali na kuhatarisha maisha yao.
Wakiongozwa Edward Kimakwa, wamesema barabara hiyo ni ndogo kwa trela hizo, wakidai zimechangia kwa visa vya ajali.
Aidha, wameibua hofu ya kupata maradhi kutokana na vumbi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































