KANU KUKATA RUFAA BAADA YA ‘KUPOKONYWA’ KICC
Chama cha KANU kimetangaza kukata rufaa uamuzi wa mahakama kuu kuamua kwamba ardhi ya jumba la mikutano KICC inamilikiwa na serikali na wala si chama hicho.
Katika taarifa saa chache baada ya uamuzi wa mahakama, KANU imesema haijaridhishwa na uamuzi huo, na kutangaza kwamba imewaagiza mawakili wake kukata rufaa.
Awali, jaji Jacqueline Mogeni ameamuru kwamba KANU ilipata ardhi hiyo kwa njia haramu, na kuongeza kwamba kwenye Ushahidi wao, KANU imeshindwa kuonyesha jinsi ardhi ya umma ilitengwa na kupewa mwenyekiti wa chama cha kisiasa
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































