HUENDA MAGAVANA WANAFUJA FEDHA ZA UMMA; SENETA OLEKINA
Seneta wa kaunti ya Narok Ledama Olekina ametaka ukaguzi wa ada ya kisheria kufanyw katika serikali zote za kaunti.
Kauli ya olekina inajiri baada ya baadhi ya magavana kukosa kufika mbele ya kamati ya bunge la seneti kufafanua matumizi ya fedha katika kaunti zao na badala yake kuwatuma mawakili wao kuwawakilisha.
Kwa mujibu wa Olekina huenda magavana hao wanatumia fedha za umma kuwalipa mawakili wao kinyume na sheria.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































