#Business

UCHUNGUZI WA SENETI WAFICHUA HASARA YA BILIONI 6.6 KATIKA SAKATA YA UAGIZAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA

Kamati ya Seneti ya Biashara imefichua njama kuhusu jinsi walipa ushuru wa Kenya walipoteza Shilingi bilioni 6.6 kati ya Shilingi bilioni 9 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kupikia.

Katika kisa cha ufisadi na usimamizi mbovu uliokita mizizi katika mfumo wa ununuzi nchini, Shirika la Biashara la Kitaifa la Kenya limekabiliwa na wakati mgumu kueleza jinsi lililazimika kuuza tena mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi chini ya bei ya soko la humu nchini.

Uchunguzi wa Kamati ya Seneti kuhusu Biashara, Viwanda na Utalii umefichua kuwa mitungi 797,564 ya lita ishirini za mafuta hayo ambazo zilikuwa zimeagizwa kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini kutokana na bei ya juu ya bidhaa ziliuzwa kwa kampuni mbili Environ Pro na EnBV Kenya ili zisafirishwe tena.

Hati zilizowasilishwa mbele ya kamati hiyo zimeonyesha kuwa mtungi moja ya lita 20ya mafuta ya kupikia , shirika hilo liliiuza kwa Shilingi 3,028, chini ya bei ambayo mafuta ya kupikia yaliuzwa kwa reja reja.

Katika kipindi hicho, kontena la lita 20 nchini Kenya lilikuwa likiuzwa kwa takriban Shiingi 5,000, na chini ya mpango huo, KNTC ilipaswa kuziuza kwa takriban Shilingi 4,800 ikiwa wangerudisha kiasi ambacho kilikuwa kimeelekezwa kwenye utoaji wa bei nafuu wa mafuta ya kula.

Wabunge walikuwa na hamu ya kufahamu ni kiasi gani kilipatikana kutokana na mauzo ya mafuta ya kupikia yaliyoagizwa kutoka nje ya nchi chini ya mpango huo.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *