#Football #Sports

HUSSEIN ASISITIZA HAKI KATIKA KURA ZA FKF

Huku uchaguzi ujao wa FKF ukikaribia kwa kasi, mgombea Urais wa FKF Hussein Mohammed ameibua wasiwasi mkubwa kuhusu uwazi na mawasiliano kutoka kwa Bodi ya Uchaguzi ya FKF.

Mohammed ameleezea kusikitishwa na kuongezeka kwa ukosefu wa taarifa za wazi kutoka kwa bodi, hasa kuhusu michakato muhimu ya uchaguzi. Ameitaka bodi ya uchaguzi kutoa taarifa za haraka kuhusu masuala kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na maeneo ya vituo vya kupigia kura na mchakato wa uhakiki wa vilabu. Katika ngazi ya mashinani. Wakati huo huo, bodi ya uchaguzi Jumatatu, ilichapisha Hati za Uchaguzi wa 2024., ikijumuisha usajili wa vilabu.

Tayari bodi ya uchaguzi imechapisha Ratiba ya Muda ya Uchaguzi ya FKF 2024 – huku Wadau wakihimizwa kuendelea kufahamishwa kuhusu hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi.

Sawia na Msimbo wa Uchaguzi wa FKF uliorekebishwa – ambao ulipitishwa na kuidhinishwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Agosti 24, 2024 na,

Mwongozo wa Uchaguzi wa FKF – ambao Bodi inasema una miongozo ya kina ambayo inahakikisha mchakato wa uchaguzi ulio wazi na wa haki.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HUSSEIN ASISITIZA HAKI KATIKA KURA ZA FKF

NYASI BANDIA ZILIHARIBU MCHEZO

HUSSEIN ASISITIZA HAKI KATIKA KURA ZA FKF

TAREHE YA NAIROBI FIGHT YATANGAZWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *