MASWALI KUHUSU KIFO CHA OJWANG’
Huku upasuaji wa maiti ya Albert Ojwang, mwanablogu aliyekamatwa na kufariki akiwa kwenye seli za polisi kwa madai ya kumchafulia jina naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Langat ukitarajiwa hii leo, maswali yameendelea kuibuliwa kuhusiana na kukamatwa kwake.
Viongozi wanaoegemea chama cha ODM wametaka kujua ni kwanini kijana huyo akasafirishwa kutoka Homa Bay hadi Nairobi, wakitaka uchunguzi wa kina kufanywa.
Wakiongozwa na Millie Odhiambo na James Nyikal, viongozi hao wamepinga madai kwamba Ojwang alijiua.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































