TUPO TAYARI KWA MSIMU UJAO ASEMA CARLO ANCELOTTI

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amesema timu yake itarejea kupata taji zaidi msimu ujao baada ya kunyakua rekodi ya kombe la 15 la Ligi ya Mabingwa huko Wembley Jumamosi.
Los Blancos waliwazima Borussia Dortmund na kisha wakafunga mabao mawili kupitia kwa Dani Carvajal na Vinicius Junior na kupata ushindi wa 2-0.
Muitaliano huyo alinyanyua kombe hilo kwa mara ya tano iliyoongeza rekodi yake.
Madrid, ambao walikamilisha La Liga na Ligi ya Mabingwa mara mbili kwa mara ya tano katika historia yao, ndio kikosi kikuu cha Uhispania.
Madrid itampoteza kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, akistaafu kucheza soka baada ya Euro 2024.
Imetayrishwa na Nelson Andati