WALIMU WA JSS WAAPA KUTOREJEA KAZINI
Shughuli za masomo katika shule za sekondari ya msingi JSS zimeendelea kulemazwa kwa wiki ya pili sasa, huku walimu wa JSS wakisema kuwa utekelezwaji wa mtaala wa elimu wa CBC utadorora iwapo serikali haitafanya kipaumbele maslahi ya walimu.
Wakiandamana katika kaunti mbali mbali nchini, walimu hao wameapa kuandamana hadi katika tume ya huduma za walimu TSC kushinikiza kuajiriwa kwa kandarasi ya kudumu.
Walimu hao vile vile wamepuuzilia mbali agizo la TSC la kutishia kuwachukulia hatua iwapo hawatarejea kazini.
Kulingana na walimu hao ambao wamekuwa wakihudumu kwa kandarasi ya muda kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa ni ukiukaji wa agizo la mahakama kutenga fedha za kuwaajiri kwa kandarasi ya kudumu.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































