KNUT SASA YAILILIA SERIKALI
Chama cha kitaifa cha kutetea maslahi ya walimu KNUT kimeitaka serikali kurejesha kima cha shilingi bilioni 10.1 zilizopunguzwa kutoka kwenye bajeti ya tume ya kuwaajiri walimu TSC katika mwaka huu wa kifedha baada ya kutupiliwa mbali kwa mswada wa fedha.
Katika taarifa, katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu amelalamika kwamba licha ya TSC kurai kamati za bajeti na ile ya elimu kutopunguza fedha hizo, serikali imepunguza mgao wa TSC kutoka shilingi bilioni 357 hadi bilioni 347.
Kwa mujibu wa Oyuu, hatua hiyo itaathiri utkelezwaji waw amu ya pili ya mkataba wao wa maelewano na TSC, ambayo itakuwa saw ana ukiukaji wa mktaba huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































