#Local News

OJWANG KUZIKWA LEO

Viongozi mbali mbali wameratibiwa kujiunga na waombolezaji katika shule ya msingi ya Nyawango kaunti ya Homa Bay katika kumsindikiza mwendazake Albert Ojwang ambaye ni bloga na mwalimu aliyeuawa mikononi mwa polisi mwezi jana.

Mwili wa Ojwang uliwasilishwa eneo hilo hapo jana, hafla iliyogeuka kuwa taharuki na ghadhabu baada ya waombolezaji kuchukua mwili wake kwa nguvu na kuelekea naye katika kituo cha polisi cha Mawengo kabla ya kukiteketeza.

Idara ya polisi nchini hadi sasa haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

OJWANG KUZIKWA LEO

WAFANYABIASHARA WAACHWA NA HASARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *