RUTO AWAPA MAGAVANA JUKUMU

Rais William Ruto amewataka magavana kuhakikisha hospitali zote za umma na za kibinafsi kwenye kaunti zao zimejiandikisha chini ya bima ya afya SHA ili kuhakikisha mpango wa serikali wa utoaji huduma za afya kwa wote UHC unatekelezwa kikamilifu.
Rais ameyasema haya kwenye mkutano na magavana katika Ikulu ya Nairobi hapo jana, akitaja hatua ya baadhi ya hospitali hizo kukosa kujiandikisha kama kikwazo kwenye mpango huo wa serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa