GAVANA MWADIME KUFUFUA UFUGAJI

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Andrew Mwadime ameeleza matumaini katika kufufua sekta ya kilimo na ufugaji
Lengo kuu la hatua hiyo kulingana na mwadime ni kuongeza mapato zaidi kwa wakulima na wafugaji wa kaunti hiyo na kwamba serikali yake imejitolea kupiga jeki sekta hiyo
Mwadime aidha amesema serikali yake imetia Saini mkataba na mwekezaji akakayekamilisha ujenzi wa kiwanda cha ndizi mjini Taveta na kwamba wameshirikiana na baadhi ya nchi za mashariki ya kati ambapo wafugaji watapata fursa ya kuwauza mifugo wao
Imetayarishwa na Janice Marete