#Local News

IG KANJA ASUKUMA MAGEUZI YA AFRIPOL KATIKA MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI NCHINI ALGERIA

Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja anaongoza majadiliano kuhusu mageuzi muhimu ndani ya Mfumo wa Umoja wa Afrika wa Ushirikiano wa Polisi (AFRIPOL) katika mkutano wa 12 wa Kamati ya Uongozi huko Algiers, Algeria.

Kanja, ambaye pia anahudumu kama Rais wa Baraza Kuu la AFRIPOL, leo hii ameongoza mashauri yaliyolenga kurekebisha sheria, utawala na bajeti ya shirika.

Mkutano huo wa siku mbili, unalenga kurahisisha shughuli za AFRIPOL kabla ya Mkutano Mkuu ujao ili kuimarisha ushirikiano wa polisi kote Afrika.

AFRIPOL inashirikiana kwa karibu na mashirika ya kutekeleza sheria kama vile INTERPOL na washirika wa maendeleo ili kupambana na uhalifu uliopangwa wa kimataifa, ugaidi na uhalifu wa mtandaoni.

Kanja ameandamana na msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) Dkt. Resila Onyango.

Mkutano huo umeuthuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Polisi wa Kitaifa wa Algeria Ali Badaoui,Mkurugenzi Mtendaji AFRIPOL Jalel Chelba, Mshauri wa Kisheria wa AU Salem Mohamed, Wakuu wa Polisi wa Afrika, Wawakilishi wa AU PAPs na HR, na Wakuu wa Ushirikiano wa Polisi wa Mikoa.

Imetayarishwa na Janice Marete

IG KANJA ASUKUMA MAGEUZI YA AFRIPOL KATIKA MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI NCHINI ALGERIA

WAKULIMA WA KAHAWA SIRISIA KUPATA HAKI, SERIKALI

IG KANJA ASUKUMA MAGEUZI YA AFRIPOL KATIKA MKUTANO WA KAMATI YA UONGOZI NCHINI ALGERIA

OCHOLLA ATIA SHAKA BODI YA UCHAGUZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *