JAMII YATAKIWA KUKOMESHA DHULUMA ZA KIJINSIA
Dhuluma za kijinsia zimeendelea kuwa donda sugu ulimwenguni kote huku wito ukitolewa kwa jamii katika siku 16 za kampeni ya kukomesha dhuluma hizo.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa UN, wanawake na wasichana 140 huuawa kila siku na wapenzi au watu walio karibu nao.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, wanaharakati nchini wameitaka serikali kutilia mkazo sheria zinazohusiana na dhuluma za kijinsia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































