AUC: WANAWAKE ODM WAMWOMBEA ODINGA
Huku uchaguzi wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC ukikaribia, viongozi wanawake katika chama cha ODM wameandaa hafla ya maombi kwa ajili ya mwaniaji wa wadhifa huo Raila Odinga ambaye pia anahudhuria hafla hiyo.
Uchaguzi huo utaandaliwa baadaye mwezi huu katika makao makuu ya Muungano wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia, Odinga akimenyana na Richard Randriamandrato wa Madagascar na Mahamoud Ali Youssouf kutoka Djibout.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































