RAILA ANGALI MCHEZONI, ODM

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amekariri kwamba kiongozi wa chama hicho Raila Odinga hajastaafu kutoka ulingo wa siasa, akipuuzilia mbali taarifa zilizodai kwamba Odinga amestaafu.
Kupitia taarifa, sifuna amezitaja habari hizo kuwa zenye nia mbaya na zenye nia ya kuwavunja mioyo wafuasi wa ODM.
Aidha, amewataka wafuasi kuzipuuza taarifa hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa