ONG’ONDO: MFANYABIASHARA KUHOJIWA NA DCI
Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanatarajiwa kumhoji mwanasiasa na mfanyabiashara wa kaunti ya Homa Bay Philip Nahason Aroko aliyewekwa korokoroni baada ya kuagizwa afike katika kituo chochote cha polisi kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were.
Nahashon aliyejisalimisha katika makao makuu makuu ya DCI usiku wa kuamkia leo, amedai kwamba polisi wameshinikizwa na gavana wa Homa Bay Gladys Wanga kumwagiza ajisalimishe.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo amesema yuko tayari kushirikiana na polisi kwenye uchunguzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































