MLINZI WA USIKU AUAWA MACHAKOS
Hofu imetanda miongoni mwa wafanyabiashara mjini Machakos wanaohofia usalama wao, baada ya mlinzi mmoja wa usiku kuuawa na majambazi waliovamia duka la nguo usiku wa kuamkia leo.
Imearifiwa kuwa majambazi wamevamia duka hilo na kupora nguo na bidhaa nyingine za thamani baada ya kumwua mlinzi huyo ambaye mwili wake umepatikana nje ya duka hilo.
Wenyeji sasa wanashinikiza usalama kuimarishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































