MWANAMKE NA BINTI YAKE WAFA KATIKA AJALI YA BARABARANI

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu ajali iliyotokea katika Kituo cha Biashara cha Sikri kilichopo barabara ya Oyugis-Sondu, eneo la Rachuonyo Kusini, Kaunti ya Homa-Bay, ambapo mwanamke mwenye umri wa kati na binti yake wamefariki baada ya pikipiki yao kugongwa na trela.
Kwa mujibu wa taarifa, Pamela Ondiek na binti yake wamefariki papo hapo, huku dereva wa bodaboda akijeruhiwa vibaya.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa Polisi wa Eneo la Rachuonyo Kusini, Philemon Saera, amesema kuwa dereva wa trela amekamatwa akiwa anajaribu kutoroka baada ya kusababisha ajali hiyo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani
Imetayarishwa na Janice Marete