KWAHERI NHIF KARIBU SHA

Wizara ya afya itachapisha hatua za kujisajili katika biya ya mpya ya afya SHA hay ani kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mamlaka ya afya ya jamii Timothy Olonyi ambaye ameongeza kuwa walio na bima ya NHIF itakuwa rahisi kwao kusajiliwa
Olonyi aidha amesema serikali kwa ushirikiano na wizara ya afya itatoa maelezo zaidi kwa wakenya kabla ya bima hiyo kuanza kutumika mwezi julai
Olonyi aidha amesema wakenye walioko katika ajira watatozwa malipo ya bima hiyo kwa mwaka badala ya mwezi mpango ambao kulingana naye utasaidia katika juhudi za kukabili baadhi ya changamoto zilizoikumba NHIF
Imetayarishwa na Janice Marete