GAVANA ACHANI KUONGOZA KONGAMANO LA MAGAVANA WANAWAKE HUKO KWALE

Gavana Fatuma Achani anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Magavana Wanawake 7 katika kaunti ya Kwale.
Achani atawaongoza Magava wenza katika uzinduzi wa kituo cha 2 cha saratani katika Ukanda wa Pwani kilichoko hospitali ya Kwale.
Kituo hicho kinalenga kupunguza dhiki ya wagonjwa wanaougua saratani hasa katika Ukanda wa Pwani.
Baadaye, Magavana hao watafululiza hadi studio za kurekodi muziki za kaunti hiyo na kisha waelekee katika uwanja wa Kwale kukagua ujenzi wa uwanja huo utakaotumika kwa sherehe za Mashujaa za mwaka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa