#Local News

WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA BOMBA LA MAJI TAKA KUPOROMOKA ENEO LA SHAURI MOYO JIJINI NAIROBI

Watu wanne wamefariki baada ya bomba la maji taka lililochimbwa kuporomoka katika mtaa wa Shauri Moyo jijini Nairobi.

Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) Dkt Resila Atieno Onyango amesema kuwa operesheni ingali inaendelea katika eneo la tukio.

Ameongeza kuwa watu watatu wameokolewa na wamehudumiwa.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, watu watatu wameokolewa na kupelekwa katika Hospitali iliyo karibu kufuatia operesheni ya pamoja ambayo imehusisha kikosi cha zima moto cha Kaunti ya Nairobi, shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na maafisa wa polisi

Imetayarishwa na Janice Marete

WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA BOMBA LA MAJI TAKA KUPOROMOKA ENEO LA SHAURI MOYO JIJINI NAIROBI

WAKAAZI WA TRANSNZOIA WAMTAKA RUTO ATIMIZE AHADI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *