MICHEZO YA KSSSA KUFANYIKA KISUMU CITY

Mashindano ya kitaifa ya Chama cha Michezo ya Shule za Sekondari Kenya (KSSSA) yamehamishwa kutoka Kaunti ya Kisii hadi Kisumu City.
Mkutano kati ya KSSSA na Wizara ya Elimu ulipata hali ya ukumbi kuu, Uwanja wa Gusii, kuwa mbaya.
Michezo hiyo itakayochezwa Julai 30 hadi Agosti 7, itashirikisha michezo ya mpira wa miguu, voliboli, netiboli, raga Sevens na michezo ya racquet.
Uwanja huo ulikuwa na mechi tatu za mashindano ya kanda lakini ulikuwa na hali ya kusuasua kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, na kuwalazimu viongozi hao kusogeza nusu-fainali iliyokuwa hatarishi kati ya Agoro Sare na Matutu PAG hadi Shule ya Upili ya Cardinal Otunga, uwanja wa Mosocho.
Mechi hiyo iliahirishwa katika dakika ya 75 kutokana na matatizo ya watu.
Katibu wa KSSSA Kaunti ya Kisii Geoffrey Nyantika kuwa mojawapo ya sababu zilizolazimu hatua hiyo ni mvua kubwa iliyosababisha uwanja kujaa maji, hivyo kutochezwa. Machafuko yaliyoshuhudiwa wakati wa mchezo wa Agoro Sare dhidi ya Matutu PAG pia yalichangia.
Imetayarishwa na Janice Marete