RUTO AJITETEA DHIDI YA VIONGOZI WA KIDINI
Wakati uo huo, Rais William Ruto mwenyewe amechukua jukumu la kuitetea serikali yake dhidi ya kauli za viongozi wa kidini za hapo jana kwamba serikali yake imejaa ubinafsi badala ya kuyashughulikia maslhai ya wakenya.
Akizungumza katika hafla ya kufuzu katika chuo kimoja jijini Nairobi, Rais amewataka viongozi wa kidini na wakenya kwa jumla kuzingatia ukweli wanapotoa taarifa kwa taifa.
Aidha, amewataka viongozi kupima athari za kauli zao kabla ya kuzitoa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































