#Football #International #Sports

ROONEY ASEMA NDOTO YAKE NI KUA KOCHA WA MANCHESTER UNITED

Kocha mpya wa Playmouth Argyle,Wayne Rooney amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba itakuwa “ndoto” yake kuinoa Manchester United katika siku zijazo.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza amerejea katika usimamizi baada ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu anayefuata wa Plymouth Argyle wiki iliyopita.

Jukumu hilo ni la kwanza kwa Rooney tangu alipotimuliwa Birmingham Januari baada ya utawala mbaya na wa muda mfupi uliodumu chini ya miezi mitatu na kupoteza michezo tisa kati ya 15 akiwa kwenye usukani wa timu iliyoshika nafasi ya sita alipofika lakini baadaye ilishuka daraja kutoka daraja la pili.

Kabla ya hapo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 aliwahi kuwa kocha wa Derby County na DC United inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka (MLS).

Rooney alikuwa na maisha mazuri ya uchezaji, akimaliza kama mfungaji bora wa muda wote wa England na Manchester United, na sasa ana ndoto ya siku moja kuchukua hatamu Old Trafford.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KOMPANY ACHUKUA USUKANI BAYERN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *