UPINZANI WATAKA LAGAT, AMIN WAKAMATWE
Naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat ameendelea kujipata chini ya shinikizo, viongozi wa upinzani wakimtaka Lagat Pamoja na mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI Mohammed Amin wakamatwe na kufunguliwa mashtaka kuhusiana na mauaji ya bloga Albert Ojwang.
Viongozi hao akiwemo Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka, Okiya Omtatah, na Eugene Wamalwa, wameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati kutatua changamoto za kiusalama humu nchini.
Aidha, Gachagua amedia uwepo wa kikosi maalum kilichobuniwa na Rais William Ruto kuendeleza utekaji nyara na mauaji.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































