#Football #Sports

WAZIRI WA MICHEZO MURKOMEN NA RAIS WA CAF MOTSEPE WAMEZURU NYAYO NA TALANTA KUKAGUA UKARABATI

Waziri wa michezo Kipchumba Murkomen pamoja na rais wa CAF Patrice Motsepe, wamezuru nyuga za Nyayo na talanta kukagua ukarabati unaeondelea kwa matayarisho ya mchuano wa chan na AFCON.

Miongoni mwa viwanja vinanyokarabatiwa ni pamoja na Moi international sports complex, Nyayo na talanta sports city iliyoko jijini Nairobi.

Kenya, uganda na tanzania ziliteuliwa na CAF mwezi Septemba kuwa wenyeji wa kombe la mataifa ya Afrika, 2027, na kuleta michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili katika Africa mashariki kwa mara ya kwanza tangu Ethiopia/ uhabeshi iliposhiriki fainali za 1976.

Mbali na hayo, Kenya vile vile watakuwa wenyeji wa African nations championships (chan) 2024.

Algeria ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwisho ya chan mwezi januari na Februari 2023.

Nchi ya Senegal ilishinda taji hilo kwa kuwafunga wenyeji kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali ya kukata na shoka.

Imetayarishwa na Kennedy Osoro

WAZIRI WA MICHEZO MURKOMEN NA RAIS WA CAF MOTSEPE WAMEZURU NYAYO NA TALANTA KUKAGUA UKARABATI

AL ALHY WAIADHIBU GOR MAHIA MABAO 3-0

WAZIRI WA MICHEZO MURKOMEN NA RAIS WA CAF MOTSEPE WAMEZURU NYAYO NA TALANTA KUKAGUA UKARABATI

TIMU YA SHABANA WAMEBORESHA MUUNDO WA BASI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *