#Sports

ALILA ATAKA GOR NA AFC KUBORESHA UONGOZI WAO

Aliyekuwa mgombea urais wa FKF Tom Alila ametoa changamoto kwa Gor Mahia, AFC Leopards na Shabana FC kuboresha mfumo wao wa uongozi kwa kupitisha bodi za kuziongoza.

Kulingana na Alila, mtindo huu wa uongozi utaweka akili timamu, uwajibikaji, na usimamizi ufaao utakaokuza viwango vya soka miongoni mwa vilabu ili kuwezesha ushindani mkali katika ligi yetu ya daraja la juu.

Alila pia amezishauri timu hizi kujifunza kutoka kwa mabingwa wa ligi hiyo Kenya Police katika masuala ya uongozi, kuwaunga mkono kufanya vyema katika michuano

ya CAF Champions League.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *