UPANZI WA MICHE KUREJESHA HADHI YA MSITU MT. ELGON
Serikali inapania kurejesha hadhi ya msitu wa Mlima Elgon ulioko kwenye kaunti ya Bungoma na Trans Nzoia kwa kupanda miche milioni 10 katika kipindi cha miaka 5 ijayo.
Akizungumza na wanahabari, naibu mkurugenzi wa idara ya misitu Charity Munyasia amesema miche hiyo itapandwa kwenye ekari 7 za ardhi ya msitu huo.
Aidha, amesema kwamba mradi huo utatoa nafasi za ajira kwa wakazi walio karibu na msitu huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































