WAZIRI MUTUA ATANGAZA KAZI NCHINI QATAR
Waziri wa Leba Alfred Mutua amekuwa akipokea msukosuko kutoka kwa umma kufuatia tangazo lake la nafasi za kazi kutoka kwa kampuni ya Qatar.
Sawa na bosi wake, Rais William Ruto, Mutua amekuwa mtetezi wa kusafirisha wafanyikazi wa ndani hadi mataifa ya kigeni ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Kenya ambacho kinafikia asilimia 12.7.
Katika tukio hili, Mutua amechapisha kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusu kampuni ya Qatar ambayo maafisa wake wako Nairobi kutafuta wafanyakazi wenye ujuzi katika nyanja mbalimbali.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































