MAAFIA 200 WA POLISI WAELEKEA HAITI

Kundi la pili la polisi wa Kenya limeondoka Nairobi kuelekea Haiti kusaidia kupambana na magenge ambayo yalikuwa karibu kulivamia taifa la Caribbean.
Timu hiyo ya maafisa 200 waliofunzwa vyema iliondoka jana Jumatatu, usiku kwa ndege ya kukodishwa na Umoja wa Mataifa na iliratibiwa kuwasili Port-au-Prince leo mwendo wa saa 10 asubuhi kwa saa za Kenya.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Utawala anayeondoka, mratibu wa Misheni ya Msaada wa Usalama wa Kimataifa nchini Haiti, Noor Gabow, na kaimu DIG James Kamau walikuwepo kuwaaga maafisa hao.
Imetayarishwa na Janice Marete