WASHIKADAU: MRADI WA NYUMBA NAFUU WARAHISISHA UMILIKI

Washikadau katika sekta ya ujenzi wametaja mradi wa nyumba za bei nafuu kama njia mojawapo ya kupunguza gharama ya kumiliki nyumba nchini na kwamba Wakenya wengi wamenufaika na mradi huo.
Wakizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 70 tangu kuzinduliwa kwa shirika la kitaifa la nyumba NHC katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, washikadau hao wamepongeza hatua ya shirika hilo kuanzisha makazi ya bei nafuu.
Kwa upande wake, katibu mkuu katika wizara ya nyumba Charles Hinga, amesema tayari nyumba za bei nafuu elfu 103 zimejengwa chini ya mpango huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa