SERIKALI YATANGAZA AFUENI MAU
Mzozo wa ardhi katika msitu wa Mau hatimaye umepata suluhu baada ya zoezi la upimaji wa msitu na kuweka mipaka baina ya msitu huo na ardhi ya wakazi kukamilika, wakazi sasa wakiratibiwa kupokezwa hatimiliki ndani ya muda wa wiki moja.
Tangazo hilo limewekwa wazi na katibu mkuu katika wizara ya ardhi Nixon Korir, akisisitiza kuwa serikali inajitahidi kumaliza vuta nikuvute za ardhi.
Ameyasema haya akiwa katika kaunti ya Baringo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































