WAKENYA KUTOA SAUTI KUHUSU ADANI

Wakenya wameratibiwa kupata fursa ya kuamua iwapo serikali itakodisha uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA kwa kampuni ya Adani au la, baada ya wizara ya kawi kupanga kuanza kuandaa vikao vya kuchukua maoni ya Kenya kuhusu mpango huo ambao umezua pingamizi kali.
Kwa mujibu wa serikali, lengo la kukusanya maoni ni kupata mitazamo tofauti ya wakenya kuhusu pendekezo la ushirikiano wa kibinafsi wa uwekezaji.
Aidha, Waziri wa kawi Opiyo Wandayi amesema wanapanga kufahamu mtazamo wa wakenya kuhusu pendekezo la kuipa kampuni ya Adani shughuli za usambazaji wa umeme humu nchini
Imetayarishwa na Antony Nyongesa