OCHOLLA ATIA SHAKA BODI YA UCHAGUZI
Mgombea urais wa Shirikisho la Soka la Kenya Sam Ochola ametilia shaka uadilifu wa bodi ya uchaguzi kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 7, 2024.
Katibu Mkuu wa Gor Mahia anaamini bodi hiyo lazima ifanye kazi kutoka kwa afisi isiyoegemea upande wowote ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi huru na wa haki.
Ochola atawania kiti cha urais wa FKF pamoja na mgombea mwenza Willis Waliaula na amejiunga na washindani wengine, akiwemo aliyekuwa mjumbe wa NEC ya Nyanza Tom Alila, mfanyabiashara Cleophas Shimanyula, zamani wa kimataifa Sammy Kempes Owino, Husein Mohammed na naibu wa rais wa sasa Doris Petra.
Ochola, hata hivyo, alisalia kujiamini katika kukuza soka nchini iwapo atachaguliwa kushika wadhifa huo. Bodi ya uchaguzi inayoongozwa na Profesa Hesbon Owillal inatarajiwa kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea urais mnamo Novemba 2 kabla ya uchaguzi.
Mgombea mwingine wa urais, Sam Nyamweya, alijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Nyamweya, ambaye awali aliwahi kuwa rais wa FKF kabla ya kukabidhi kijiti kwa Nick Mwendwa, alisema kuwa uamuzi huo umefanywa baada ya ‘kutafakari na kushauriana kwa kina’.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































