BILA BILION KUMI NA MBILI EZE HAONDOKI
Crystal Palace haitafikiria kumuuza Eberechi Eze kwa punguzo la Shilingi bilioni 12 kifungu cha kutolewa kwenye mkataba wa mchezaji huyo, gazeti la The Mirror limeripoti.
Haya yanajiri huku Arsenal ikionyesha nia ya kumnunua kiungo huyo, ambaye sasa anaibukia kama shabaha kubwa ya klabu hiyo katika dirisha hili.
Eze amefurahishwa na uwezekano wa kuhamia kwa wababe hao wa London kaskazini – ambako alianza safari yake ya soka, kwani ana matarajio ya kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Tottenham Hotspur pia wameonyesha nia, lakini Arsenal wako mbele katika mbio hizo
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































