NIMENAWA MIKONO

Vikao vya kusikiliza hoja ya kumwondoa afisini Waziri wa kilimo Mithika Linturi kutokana na Sakata ya mbolea ghushi vimekamilika leo hii.
Mbunge wa Bumula Jack Wamboka ambaye ndiye aliyewasilisha hoja hiyo bungeni ameiomba kamati inayochunguza hoja hiyo kuhakikisha kwamba Linturi ameondolewa afisini.
Akiwasilisha hoja yake ya mwisho mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na mbunge maalum Naomi Waqo,wamboka amesema wakenya wengi hasa wakulima wanakadiria hasara kutokana na utepetevu wa Waziri Mithika Linturi.