WAKENYA WACHUNGULIA IEBC MPYA
Mchakato wa kubuniwa upya kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC umepiga hatua kubwa, Rais William Ruto akipokezwa rasmi ripoti ya jopokazi lililoendesha zoezi la kuwapiga msasa wanaowania kuhudumu kama mwenyekiti na makamishna wa tume hiyo.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amelipongeza jopokazi hilo, akiahidi kuhakikisha wanaoteuliwa kuhudumu ni watu walio na vigezo hitajika.
Jopokazi hilo linaongozwa na mwenyekiti wake Dakta Nelson Makanda.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































