#Local News

WAZIRI OGAMBA AONYA WANAOJARIBU KUDANGANYA MTIHANI WAKATI KCSE INAENDELEA


Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa onyo kali kwa yeyote anayenuia kudhoofisha uaminifu wa mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE) ambao unaendelea kote nchini.

Jumla ya watahiniwa 965,501 wamejiandikisha kwa mtihani wa mwaka huu katika vituo 10,754 nchini kote na kulingana na Waziri, wale watakaopatikana wakijihusisha na udanganyifu hawatasamehewa. Ogamba alithibitisha kuwa karatasi zote za mtihani ziko salama na zimehifadhiwa vizuri, akikanusha ripoti kwamba baadhi ya vifaa viko kwenye mzunguko.

Ingawa baadhi ya karatasi kama Ushonaji na Kompyuta zilifanywa wiki iliyopita, leo inaashiria mwanzo rasmi wa zoezi la kitaifa na watahiniwa wanatarajiwa kufanya mtihani wa Kiingereza na kemia.

Imetayarishwa na Janice Marete

WAZIRI OGAMBA AONYA WANAOJARIBU KUDANGANYA MTIHANI WAKATI KCSE INAENDELEA

TIMU YA CHUO KIKUU CHA PEERLESS KABARAK

WAZIRI OGAMBA AONYA WANAOJARIBU KUDANGANYA MTIHANI WAKATI KCSE INAENDELEA

SHEILA CHEPKIRUI AIBUKA KIDEDEA KWA OBIRI KUWANIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *