MUDAVADI: KENYA, UCHINA KUSHIKAMANA ZAIDI
Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amesema kwamba serikali ya Kenya inalenga kuboresha uwekezaji kati yake na Uchina kwa lengo la kuimarisha biashara na mshikamano baina ya mataifa hayo mawili.
Akizungumza katika ubalozi wa taifa hilo jijini Nairobi, Mudavadi amesema kwamba hatua za uwekezaji na ushiriikiano kwenye miradi mbali mbali umesaidia kenya kupiga hatua za kimaendeleo, na kuyataka mataifa mengine kuiga mfano huo.
Naye balozi wa Uchina humu nchini Zhou Pingjian amesema Uchina itaendelea kuimarisha ushirikiano huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































