OTERE APANIA KUNYAKUA TAJI LA MPIRA WA WAVU
Kocha mkuu wa Klabu ya Mpira wa Wavu ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya James Ontere analenga kusaidia klabu hiyo yenye makao yake makuu mjini Mombasa kunyanyua taji lao la kwanza watakapomenyana na mabingwa wa rekodi ya GSU katika fainali inayotarajiwa kufanyika Juni 6-8, 2025, uwanaj wa ndani wa Kasarani.
Ontere anasalia na furaha kuhusu kuandikisha historia akiwa na KPA baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi Kenya Prisons katika nusu-fainali.
Mshambulizi huyo wa zamani anasema maandalizi yameshika kasi na ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kuwekeza kwenye timu ili kuwa na maandalizi ya hali ya juu.
Ontere anasema wanafanya mazoezi ya jinsi ya kukabiliana na uchezaji wa GSU huku wakipiga msasa udhaifu wao ili kutawala katika fainali.
Fainali itachezwa katika mfumo wa msururu wa michezo mitatu bora.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































