JOPOKAZI LA KUCHUNGUZA DHULUMA LAAPISHWA
Kitendawili cha mauaji yanayokisiwa kuwalenga wanawake kinatarajiwa kuteguliwa hivi karibuni baada ya jopokazi la kuchunguza visa hivyo chini ya uwenyekiti wa aliyekuwa naibu jaji mkuu Nancy Barasa kuapishwa.
Mauaji hayo yameibua hofu nchini, takribani wanawake 170 wakiripotiwa kuuawa mwaka uliopita, katibu katika wizara ya usalama Raymond Omollo akilitaka jopokazi hilo kusaka suluhu mara moja.
Kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa hapo jana, wanawake 100 waliuawa na watu wanaofahamiana nao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































