BUNGOMA QUEENS WAINGIA FAINALI
KLABU ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-WPL) Bungoma Queens imepania kutinga fainali ya Kombe la Wanawake la FKF baada ya kung’oa Trinity Starlets katika robo-fainali wikendi.
Ushindi wao uliifanya Bungoma Queens kuchuana na Vihiga Queens katika nusu fainali iliyotarajiwa kuchezwa Alhamisi.
Bungoma Queens, ambao wameimarika kwa kasi katika kipindi chote cha dimba, watatafuta kutumia fomu yao ya hivi majuzi na nidhamu ya kimbinu ili kuwashinda mabingwa hao mara tatu wa Ligi Kuu ya Wanawake.
Queens itategemea ubunifu wa fowadi wao hatari Catherine Khaemba kwa mabao.
Mshindi wa pambano la Alhamisi atafuzu kwa fainali ya Kombe la Wanawake la FKF, ambapo watamenyana na mshindi wa pambano lingine la nusu fainali kati ya Kenya Police Bullets na Kibera Soccer Women.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































