#Sports

MANCHESTER UNITED WALEGEZA KAMBA KUHUSU MBEUMO

Manchester United wamepunguza kuhusu harakati zao za kumnasa Bryan Mbeumo licha ya kufahamu kuwa Tottenham ina nia ya kumnunua fowadi huyo wa Brentford.

Mbeumo anadaiwa kuvutiwa na Spurs, ambao wamemteua bosi wake wa zamani Thomas Frank, lakini hali ilivyo sasa inoanekana anaelekea United.

United wanatarajiwa kurejea na ofa nyingine kwa Mbeumo baada ya dau lao la awali la hadi £55m kukataliwa.

Inabakia kuonekana iwapo Tottenham watafuatilia mazungumzo yao ya awali au watahamia kwa Antoine Semenyo wa Bournemouth.

Brentford inamthamini Mbeumo, ambaye kwa hakika amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake, kwa zaidi ya pauni milioni 60 na wako tayari kusikiliza ofa.

United wana malengo mengine kwenye nafasi ya Mbeumo, akiwemo Semenyo, na wana maadili yao wenyewe akilini kwa wachezaji wote wawili.

Wakati huohuo Florian Wirtz anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Liverpool siku ya Ijumaa ili kukamilisha uhamisho wake uliovunja rekodi ya Uingereza kwenda Anfield.

Huku Uhamisho wa Adrien Truffert wa £14.4m kutoka Rennes kwenda Bournemouth unatarajiwa kufungua njia kwa Milos Kerkez kujiunga na Liverpool.

Napoli wanachunguza kumnunua winga wa Man Utd Jadon Sancho na pia mshabuliaji wa Liverpool Darwin Nunez,

Chelsea wamefanya mawasiliano ya awali na Lyon kumnunua winga Malick Fofana.

Leeds wanakaribia kuinasa saini ya beki wa kati wa Udinese, Jaka Bijol.

Klabu ya Crystal Palace iko tayari kutangaza kumsajili mlinda mlango Walter Benitez siku chache zijazo.

Diego Coppola amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa Brighton kabla ya uhamisho wake kutoka klabu ya Serie A ya Hellas Verona.

Celtic wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa kati wa Albirex Niigata, Hayato Inamura.

Imetayrishwa na Nelson Andati

MANCHESTER UNITED WALEGEZA KAMBA KUHUSU MBEUMO

SEVILLA WAPATA KOCHA MPYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *