#Athletics #Sports

BADO NAPUMZIKA

Bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 800 Keely Hodgkinson amefichua kwamba yuko mapumzikoni kwa salio la msimu huu baada ya kupata jeraha.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 alikua mwanamke wa tatu wa Uingereza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za mita 800 huko Paris mwaka huu akifuata nyayo za Anne Packer mwaka wa 1964, na Kelly Holmes mwaka wa 2004.

Huo ulikuwa ushindi wake wa tisa katika mbio tisa msimu huu na amesisitiza kuwa ametimiza yote aliyolenga mwaka huu.

Lengo lake kuu linalofuata litakuwa kushinda taji la dunia kwa mara ya kwanza huko Tokyo mnamo 2025.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BADO NAPUMZIKA

DCI YATANGAZA ZAWADI KUHUSIANA NA KHALISIA

BADO NAPUMZIKA

KALULU AJIUNGA NA JUVENTUS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *