TIKIKITI ZA OLYMPIC ZANUNULIWA KWA WINGI

Waandalizi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris wamesema kwamba bado zimesalia tiketi milioni 1.2 kwa Michezo hiyo, nyingi zikiwa za mpira wa miguu, mpira wa vikapu na mpira wa mikono.
Michezo ya timu kama vile kandanda imetatizika kuuza tiketi za viwanja vikubwa vilivyochaguliwa kwa ajili ya mechi hiyo, huku waandaji pia wakipanga kutoa nafasi mpya zinazotafutwa zaidi kwa fainali za kuogelea na riadha kuanzia leo hii.
“Zaidi ya tiketi 50,000 zitauzwa kwa zaidi ya michezo 30 (hii leo),” kulingana na naibu mkurugenzi mkuu Mickael Aloisio.
Michezo ya Paris imeweka rekodi mpya kwa jumla ya tiketi zilizouzwa, huku tikiti milioni 8.7 zilizonunuliwa zikipita ile ya juu zaidi ya milioni 8.3 kwenye Michezo ya Atlanta mnamo 1996.
“Zaidi ya asilimia 60” ya tikiti zimeuzwa nchini Ufaransa, Aloisio alisema.
Waandalizi walikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa mashabiki na hata baadhi ya wanariadha kuhusu gharama ya tiketi zilipotolewa kwa mara ya kwanza mwaka jana, jambo ambalo lilitia doa ahadi kwamba hii ni “Olimpiki ya watu wa kawaida”.
Imetayarishwa na Nelson Andati