#Business

UAJIRI SHA WAPIGWA BREKI

Mahakama ya uajiri na leba imetoa pigo kwa mchakato wa uajiri wenye utata wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) baada ya kutoa uamuzi kwamba matangazo yake ya ndani yaliyokuwa yanawahusu waliokuwa wafanyakazi wa Bima ya Afya ya taifa (NHIF) yalikuwa ya kibaguzi na kinyume na Katiba.

Jaji Byram Ongaya, akitoa uamuzi katika ombi lililowasilishwa na mlalamishi wa maslahi ya umma Said Omar Abdile, ametangaza kuwa SHA ilikiuka masharti ya kikatiba kuhusu utendaji wa haki wa kazi, usawa, na uwazi.

Mahakama imekataza SHA kuendelea na uajiri uliochapishwa Machi 2025 na kuagiza kuwa nafasi zote zitangazwe tena kwa ushindani na uwazi.

Abdile alipinga hatua ya SHA ya kuweka kikomo maombi ya nyadhifa kadhaa za juu, ikiwa ni pamoja na Wakurugenzi, Waratibu wa Kaunti, na Maafisa wa Uhakiki Ubora, kwa wafanyikazi wa zamani wa NHIF, akisema mchakato huo haukuwa na haki na ushirikishwaji.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *