HAKUNA WIZI WA MTIHANI, WIZARA YAKANA
Huku uadilifu wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha 4 KCSE ukitiliwa shaka kutokana na visa vya udanganyifu, serikali imesema kwamba mtihani huo uko salama kwamba hakujakuwa na udanganyifu wowote.
Akizungumza kwenye kaunti ya Meru mapema leo, katibu katika wizara ya elimu Dakta Belio Kipsang amesema majaribio ya wizi yamezimwa huku akiongeza kuwa karatasi za mtihani ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni ni ghushi.
Aidha Kipsang ametoa hakikisho kwamba masomo ya gredi ya 9 yanayoanza Januari yataendelea bila tashwishwi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































