ELIZABETH CHESANG TATU TENA

Mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu NCPD Elizaeth Chesang ameongezewa muda wa kuhudumu katika wadhfa huo kwa miaka mitatu Zaidi,
Chesang ambaye alipaswa kukamilisha muda wake wa kuhudumu tarehe mbili mwezi huu wa mei ameongezewa muda wa kuhudumu na rais William Ruto.
Kupitia kwa gazeti rasmi la serikali , chesang aliteuliwa tarehe 7mei mwaka huu na amekuwa akuhudumu kama mwenyekiti wa NCPD tangu juni tarehe 23 mwaka uliopita alipoteuliwa kuchukua nafasi ya Peter Muchiri ambaye uteuzi wake ulitwaliwa.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































